Tatizo ni Barbara kuwa Mtendaji Simba au kuna jingine?

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Sep 2020
Tatizo ni Barbara kuwa Mtendaji Simba au kuna jingine?

Baada ya uteuzi wa Mtendaji Mkuu mpya wa Simba kutangazwa hapo jana, mjadala mkali umeibuka kwenye mitandao ya kijamii, Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamis Kingwangalla akiongoza mjadala huo

Dk Kigwangalla ameonekana kutokubaliana na uteuzi wa Barbara Gonzalez ambaye kabla ya kupewa majukumu hayo, alikuwa Mtendaji wa Mo Dewji Foundation pamoja na kufanya kazi nyingine kama Msaidizi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ambaye ndiye Mwekezaji wa klabu ya Simba, Bilionea Mohammed Dewji

Mjadala huo ni kama umetoka kwenye hoja ya Msingi ambayo ni uteuzi wa Barbara

Sijafahamu tatizo liko wapi katika uteuzi wa Barbara. Huyu ni Mwanamama msomi na mwenye uzoezu wa kuongoza Taasisi kubwa

Siamini kama Bodi ya Wakurugenzi inaweza kukurupuka kumteua yeye kuchukua majukumu yaliyoachwa na Senzo Mazingiza

Hata Mazingiza alipoondoka, aliyekuwa akishika nafasi yake ni huyuhuyu Barbara, amefanya kazi ya Kukaimu kwa mwezi mzima

Nadhani hili ni jambo ambalo halipaswi kuwashughulisha sana Wanasimba, Barbara apewe muda afanye kazi kama kutakuwa na mapungufu yataonekana

Masuala ya mchakato wa uwekezaji yamejadiliwa sana, na imeelezwa kuwa mchakato bado haujakamilika

Imeelezwa pia Bilioni 20 zipo, zinasubiri tu mchakato huo ukamilike lakini muhimu zaidi Mo amekuwa akitoa takribani Bilioni 3 kila mwaka kwa ajili ya uendeshaji wa timu

Haya ni masuala ambayo Wanasimba wanayafahamu, na hayawezi kuwasumbua kwani klabu mpaka sasa iko kwenye mikono salama, imeendelea kupata mafanikio

Leo msimu mpya wa ligi kuu unaanza, Wanasimba wasitolewe kwenye 'reli' kwa mijadala hii isiyokuwa na Afya

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’