Kesho Jumapili msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom unaanza kwa viwanja kadhaa kuwaka moto
Moja ya mechi zinazosubiriwa kwa hamu, ni mchezo kati ya mabingwa watetezi Simba dhidi ya Ihefu Fc vijana waliopanda daraja kupitia play-off baada ya kuiondosha Mbao Fc kwa faida ya mabao ya ugenini
Ni kama Ihefu Fc wanaanza msimu na bahati mbaya kwani wamepangwa na kuanza na wekundu hao wa Msimbazi ambao tangu mwezi wa nane hawajapoteza mchezo wowote
Kocha Mkuu wa Ihefu Fc Maka Mwalwisi amesema wanatambua wanakwenda kukumbana na vigogo, mabingwa watetezi ambao wako katika ubora wa hali ya juu
Amesema wataiheshimu Simba lakini watapambana kusaka matokeo katika mchezo huo
"Baada ya kupanda daraja tulifahamu tutakutana na timu zote za ligi ikiwemo Simba. Tunawaheshimu kwa sababu ni mabingwa watetezi na wana timu nzuri, lakini tutacheza nao kama tutakavyofanya kwa timu nyingine zote. Muhimu tunahitaji kupata matokeo mazuri kwenye uwanja wetu wa nyumbani," alisema Maka
Simba wako mkoani Mbeya tangu Jumanne wakijiwinda na mchezo huo ambao wamepania kuanza ligi kwa kishindo kwa kuondoka na alama zote tatu