Kiungo mpya wa Simba Larry bwalya ameeleza kufurahia maisha ndani ya kikosi cha mabingwa hao wa nchi, akiwaahidi mashabiki kuwa ataifanyia mambo makubwa timu hiyo
Nyota huyo aliyetua Msimbazi akipokwa kimafya mikononi mwa klabu ya Yanga, amesema mapokezi aliyoyapata katika klabu hiyo ni jambo la kipekee linalomfanya ajihisi kuwa na deni kubwa kwa machampioni hao wa Taifa
"Kila ninapoingia uwanjani najiona kuwa na deni kubwa kwa sababu mashabiki wa Simba wameonyesha kuwa na imani kubwa nami. Siwezi kuwaangusha, nitahakikisha najituma kila nitakapopewa nafasi ili kuwapa furaha," Bwalya aliuambia mtandao wa Simba
Bwalya yuko na kikosi cha Simba mkoani Mbeya wakiwa tayari kuikabili Ihefu kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu siku ya Jumapili
Hakuna shaka, Bwalya anaweza kuwa sehemu ya wachezaji 14 ambao wanaweza kupata nafasi ya kucheza