Sven apania kuanza kibabe Mbeya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Sep 2020
Sven apania kuanza kibabe Mbeya

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa soka Tanzania bara, Simba Sven vandenbroeck amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo wa ufunguzi ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2020/21 dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya

Kikosi cha Simba kiko mkoani Mbeya tangu juzi kikijiandaa na mchezo huo dhidi ya wageni hao waliopanda daraja msimu uliopita

Akizungumza baada ya mazoezi yaliyofanyikwa uwanja wa Sokoine jana jioni, Sven alisema ana matumaini makubwa kuwa wataanza ligi hiyo vizuri kutokana na ubora wa kikosi chake ingawa alikiri ushindani utakuwa mkubwa

"Natambua mchezo utakuwa mgumu, lakini ninajivunia vipaji na morali kwa wachezaji wangu, ninaimani tutapigana kuweza kupata pointi tatu," alisema Mbelgiji huyo.

"Jambo zuri ni kwamba hatuna majeruhi, kila mmoja yupo sawa, kila mmoja yupo tayari kucheza, hivyo nina nafasi ya kuchagua kati ya wachezaji wote niliona"

Simba imewasili jijini Mbeya ikiwa na kikosi cha nyota 25 tayari kwa mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wakuvutia kutokana na maandalizi yaliyofanywa na timu zote.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’