Kumekuwa na tetesi nyingi zinazomuhusu mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere ambaye sasa ana changamoto ya kupata nafasi kwenye kikosi cha kocha Sven Vandenbroeck
Achana na uzushi uliosambazwa jana, kumekuwa na tetesi zinazomuhusisha Mnyarwanda huyo na klabu ya APR ya huko kwao Rwanda
Hata hivyo ni wazi, Kagere hawezi kuondoka Simba wakati huu kutokana na ukweli kuwa bado anahitajika licha ya kuwa na mkataba wa muda mrefu
Simba itashiriki michuano ya ligi ya mabingwa, inahitaji safu kali ya ushambuliaji, Kagere ndiye mshambuliaji kinara katika kupachika mabao hapa Tanzania kwa misimu miwili mfululizo
Kinachopelekea akose nafasi sasa ni kwa kuwa kocha Vandenbroeck amebadili mfumo wa uchezaji wa kikosi chake, akitumia viungo watano na mshambuliaji mmoja
Katika moja ya mahojiano yake karibuni, Sven alisema mfumo anaotumia sasa unaipa timu yake uhuru wa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi kuliko ule wa washambuliaji wawili aliokuwa akiutumia awali
Sven alikiri kwa sasa mshambuliaji chaguo la kwanza ni Bocco lakini washambuliaji wengine pia watakuwa wakipata nafasi kulingana na mahitaji ya mchezo husika
Kagere bado ni mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Simba, hakuna namna mabingwa hao wa nchi watamruhusu aondoke