Ni msimu mwingine ambao Wanamsimbazi wana matarajio makubwa kwa timu yao
Hesabu ni zilezile za msimu uliopita, Ngao ya Jamii tayari, bado ligi kuu na kombe la FA
Kuna kingine kimeongezeka msimu huu, ile heshima ya kutikisa vigogo kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika lazima irejee
Msimu uliopita Simba iliondoshwa katika hatua za awali na UD Songo katika mchezo ambao hakuna aliyekuwa aiyatarajia matokeo yale
Lakini msimu huu, lengo la kwanza ni kutinga hatua ya makundi, halafu mengine yatategemea na mipango itakavyokuwa katika hatua hiyo
Ni mabingwa wa nchi Simba na Namungo Fc ambao wataenda kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya CAF msimu huu
Majirani zetu wasihofu, msimu ujao watacheza tena kwa mbeleko yetu kama ilivyokuwa msimu uliopita...!