Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba, kimewahi mkoani Mbeya mapema kujiwinda na mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom ambapo siku ya Jumapili wataikabili Ihefu Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine
Wababe hao wa soka Tanzania, siku ya jana walianza program za maandalizi ya mchezo huo mkoani Mbeya chini ya kocha mkuu Sven Vandenbroeck

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema vijana wako tayari, wana ari ya kuanza msimu kibabe kwa kuondoka na alama zote tatu Mbeya
"Kikosi kinaendelea vizuri kwa kweli, tunashukuru leo tuliwasili salama hapa Mbeya na jana tulianza mazoezi ambayo tunafanya mara mbili kwa siku
"Kila mchezaji yupo katika hali nzuri ukimwondoa Kameta peke yake mwenye majeruhi," alisema Rweyemamu.
Rweyemamu aliongeza kuwa wachezaji wote wameelekeza nguvu na akili yao kwenye Ligi Kuu Bara na wanashangazwa na taarifa za ugomvi kutokea kwenye kambi yao kati ya mshambuliaji, Meddie Kagere na kocha, Sven Vandenbroeck