Simba kufanya kweli uwanja wa Taifa leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Feb 2018
Simba kufanya kweli uwanja wa Taifa leo
Kikosi cha Simba kinashuka leo kwenye uwanja wa Taifa kukabiliana na Ruvu Shooting kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 16.

Simba vinara wa ligi watakuwa wanasaka alama tatu muhimu ili kuendelea kukaa kileleni kwa tofauti ya alama tano dhidi ya Azam FC ambayo ina alama 33 baada ya kuichapa Ndanda FC kwa mabao 3-1 jana.

Aidha Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza.

Hata hivyo mchezo wa leo huenda ukawa tofauti kwa kuwa Ruvu Shooting inaonekana kuimarika huku pia ikiwa na wachezaji wake waandamizi waliokosa mchezo wa kwanza baada ya kwenda Burundi kushiriki mashindano ya majeshi.

Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo na anatarajia ushindi mnono kama ilivyokuwa kwenye mchezo uliopita.

Kinara wa mabao Emanuel Okwi na John Bocco wanatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Simba.

Wawili hao wameifungia Simba mabao 19.

Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema kikosi chao kipo kamili na wamejipanga kuhakikisha wanamzuia 'mnyama' kwenye uwanja wa Taifa leo.

"Sisi tuko kamili, tumejipanga sawasawa," amesema Bwire.

"Tunawataka mashabiki wetu wajitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa bila woga, leo ni siku yetu ya kulipa kisasi."

Ushindi utaiwezesha Simba kufikisha alama 38 hivyo kuwa mbele ya Azam FC na Yanga ambazo zimeshinda michezo yao ya mzunguuko wa 16
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’