Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema hana tatizo lolote na mshambuliaji Meddie Kagere
Aidha Sven ameeleza kushangazwa na uzushi ulioenezwa kwenye mitandao ya kijamii unaodai kuwa alipigana na mfungaji bora huyo wa VPL kwa misimu miwili mfululizo
Sven amesema hana kawaida ya kujishughulisha na mambo yasiyo ya msingi hivyo amewataka Wanasimba wapuuze uzushi unaoenezwa
"Siwezi kutumia nguvu kwenye mambo yasiyo ya maana ambayo sijui yanatoka wapi. Mimi sina tatizo, Medie hana tatizo hilo ndilo ninaweza kusema," alisema
ADVERTISE HERE