Mshambuliaji wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere amesema amesikitishwa na taarifa zilizosambaa mtandaoni kuwa amempiga kocha wa timu hiyo, Sevn Vandenbroeck
Jana taarifa za Kagere kudaiwa kumpiga kocha huyo kisa kikiwa ni kutopangwa kikosi cha kwanza cha Simba zilizagaa kwa kasi mitandaoni
Akizungumza na EA Radio, Kagere alisema alishangaa baada ya kuona mambo hayo yanasambaa wakati yeye hajafanya tukio hilo na yuko freshi kabisa na kocha
"Kuna mambo huwa yanasemwa kuhusu mimi ambayo siyo ya kweli yenye lengo la kunichafua ndiyo maana sijawahi kuwajibu"
"Lilianza la hirizi nikanyamaza na sasa limekuja la mimi kupigana na kocha kitu ambacho siyo kweli. Tangu tumefika Mbeya hatujafanya mazoezi na leo muda huu ndiyo tunafanya sasa nashangaa sijui mwalimu nimempiga wapi," alisema Kegere.