Simba yaanza mawindo ya Ihefu Fc Mbeya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Sep 2020
Simba yaanza mawindo ya Ihefu Fc Mbeya

Kikosi cha mabingwa wa nchi, Simba kiliwasili jijini Mbeya jana wakitua jijini humo na lengo moja tu, kuanza msimu kibabe dhidi ya Ihefu Fc siku ya Jumapili katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Sokoine

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema mwanzoni mwa msimu kila timu ina nafasi sawa ya kufanya vizuri hivyo wanatarajiwa ushindani utakuwa mkubwa

Sven pia ameeleza kufuatilia usajili uliofanywa na timu nyingine, kila timu imejipanga kufanya vizuri kwenye michezo ya awali

Mbelgiji huyo amesema timu itakayopata ushindi katika mechi zake za kwanza, ndiyo itajiweka kwenye mazingira mazuri kwenye mbio za ubingwa na wachezaji wake watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kupambana.

Kocha huyo alisema licha ya kikosi chake kuwa na nyota wenye uwezo, hakuna mchezaji ambaye ana namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza, hivyo nyota wote watalazimika kujituma ili kupata nafasi ya kucheza.

"Tutaelekea kwenye mechi ya ligi, tuko tayari, tunajua hakuna mechi rahisi mbele yetu, sisi ndio mabingwa wa msimu uliopita, tunatakiwa kuendeleza ubora wetu, tunahitaji kujiimarisha kila siku," alisema

Naye Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema leo timu imeanza programu maalumu kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Ihefu.

"Tunatarajia kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Sokoine, huenda tukawa na vipindi viwili kwa siku au kimoja, kesho (leo) asubuhi tutakabidhiwa na kocha mkuu, kwa kifupi timu iko tayari kwa mapambano, kila mechi kwetu ni muhimu, hatutadharau mchezo wowote," Rweyemamu alisema.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’