Mapema leo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji aliomba kukutanishwa na shabiki wa klabu ya Simba ambaye video yake ilikuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii
Video hiyo ilikuwa ikimuonyesha shabiki wa Simba akishambuliwa na kuchaniwa jezi na mashabiki wa Yanga juzi kwenye Tamasha lao
Shabiki huyo anaitwa Kindio Hassan, amekutanishwa na Mo leo
Kindio amekabidhiwa jezi mpyaa na Bosi huyo wa Simba
"Nimefurahi kukutana na wewe leo Bw. Kindio Hassan. Pole sana na changamoto uliokutana nayo," aliandika Mo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
ADVERTISE HERE