Mchezo wa kwanza wa ligi kati ya Yanga dhidi ya wapinzani wao Simba unaotarajiwa kupigwa Oktoba 28, utachezwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Yanga ambayo ni mwenyeji wa mchezo huo ilipeleka maombi kwenye Bodi ya Ligi kuomba mchezo huo uchezwe katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza lakini Bodi ya Ligi imekataa maombi hayo.
Mtendaji Mkuu Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesisitiza kwamba Γ’β¬ΕUamuzi wa bodi umezingatia kanuni ya sita (kanuni ndogo ya sita) kuhusu uwanja ambapo mamlaka ya mwisho kuhusiana na mechi kuhama au haihami inabaki kwa bodi ya ligi na TFF.Γ’β¬Β
Timu hizo zinatarajiwa kukutana Oktoba 28 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku Yanga ikiwa na kumbukumbu kuikosa Ngao ya Jamii iliyonyakuliwa na Simba msimu huu.

ADVERTISE HERE