Hatma ya vibali vya Maproo Simba Jumatatu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Aug 2020
Hatma ya vibali vya Maproo Simba Jumatatu

Uongozi wa klabu ya Simba umethibitisha kuwasilisha maombi Wizara ya Kazi kwa ajili ya kuwaombea vibali vya kufanya kazi nchini wachezaji wao wa kigeni waliosajiliwa katika dirisha hili la usajili

Wachezaji hao walioombewa vibali ni pamoja na Mghana Bernard Morrison, Mkenya Joash Onyango, Chris Mugalu (DR Congo) na Mzambia Rally Bwalya.

Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe, amesema klabu imefuata taratibu zote hivyo wanasubiri kujibiwa na wizara husika.

"Tumepeleka maombi yetu katika mamlaka husika ya kuomba vibali vya kazi kwa wachezaji wetu wa kigeni akiwamo Morrison, mchakato huo unaendelea," alisema Kashembe.

Naye Msemaji wa Idara ya uhamiaji, Paul John Mselle alisema wao wanatoa vibali vya makazi baada ya mhusika kupata kibali cha kazi.

Alipoulizwa Kamishna wa Kazi, Andrew Mwaluisi, alisema: "Tumepokea maombi mengi ila tusubiri Jumatatu tutajua."

Vibali hivyo inapaswa vipatikane kabla ligi kuanza wiki ijayo kwani nyota hao hawataruhusiwa kucheza kama hawatakuwa na vibali vya kufanya kazi nchini

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’