Mabingwa wa nchi Simba wako mkoani Arusha tayari kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi Namungo Fc ambao utapigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Leo vijana wa kocha Sven Vandenbroeck watakuwa na nafasi ya kufanya maandalizi yao ya mwisho kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid
Simba imetawala soka la Tanzania kwa misimu yote mitatu iliyopita, hii inaweza kuwa Ngao yao ya nne mfululizo kama wataibuka na ushindi dhidi ya Namungo ambayo walikutana nayo mapema mwezi huu kwenye mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1
kocha Sven amesema hii ni nafasi yao kuhesabu taji la kwanza msimu huu, akitamba kuwa na kikosi imara baada ya usajili uliofanyika
ADVERTISE HERE