Wababe wako tayari kwa msimu mpya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Aug 2020
Wababe wako tayari kwa msimu mpya

Kikosi cha mabingwa wa soka wa Taifa hili Simba, jioni ya leo kinaondoka kuelekea mkoani Arusha tayari kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo Fc

Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Kinachowafurahisha mashabiki wa Simba ni kukamilika kwa kikosi chao ambacho kimesheheni mafundi kwelikweli

Usajili wa wachezaji kama Bernard Morrison, Larry Bwalya, Joash Onyango na wengine wapya kumeifanya Simba izidi kuwa bora zaidi

Kocha Mkuu wa Mabingwa hao wa nchi Sven Vandebroeck amekiri kuwa atakuwa na wakati mgumu kuamua wachezaji 11 wa kuanza kwani kikosi chake kimesheheni kila idara

Simba imecheza mechi tatu za kujipima mpaka sasa na imefunga mabao 14!

Walianza kwa kuichapa Vital'o mabao 6-0 mchezo wa Simba Day, wakawalaza KMC 3-1 na Transit Camp 5-2 katika mechi zilizopigwa siku moja

Wanakwenda Arusha wakiwa na kikosi kamili ambacho jana Luis Miquissone na Paschal Wawa waliongezeka

Hakuna ubishi, huu unaweza kuwa msimu mwingine wa mataji kwa wekundu hao wa Msimbazi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’