Ushindani wa namba utatuimarisha zaidi - Kahata

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Aug 2020
Ushindani wa namba utatuimarisha zaidi - Kahata

Pamoja na wengi kuamini kuwa nafasi yake ipo rehani baada ya Simba kumsajili Mghana Bernard Morrison, kiungo fundi wa Simba, Mkenya Francis Kahata, amesema upana wa kikosi hicho cha mabingwa wa Ligi Kuu Bara utachangia ushindani wenye tija ndani ya timu

Katika dirisha hili la usajili Simba imesajili nyota wapya saba, wazawa watatu, mabeki Ibrahimu Ame, David Kameta 'Duchu' na straika Charles Illamfya, huku wa kimataifa wakiwa wanne ambao ni beki Mkenya Joash Onyango, mshambuliaji Mkongomani Chris Mugalu, na viungo Mzambia Larry Bwalya na Morrison, ambaye anaonekana kutishia namba ya Kahata katika kikosi cha kwanza.

Lakini Kahata amesema kikosi cha Simba kimesheheni wachezaji wengi wazuri ambao pia wanacheza timu za taifa wanapotoka, hivyo kwake anaona ni vizuri katika kuongeza ushindani wa namba.

Kiungo huyo alisema upana wa kikosi msimu uliopita ulikuwa chachu ya kushinda mataji matatu, jambo ambalo litaongezeka zaidi msimu huu kutokana na kikosi kuimarishwa.

Msimu uliopita tulitwaa Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

"Simba ina kikosi kipana kilisheheni wachezaji wengi wazuri ambao pia wanachezea timu zao za taifa,”Kahata ambaye msimu uliopita alifunga mabao manne kwenye Ligi Kuu Bara ikiwemo pia kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi Desemba, aliiambia tovuti ya klabu hiyo.

Jumapili, August 30 Simba itashuka katika dimbani la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Jumapili kuvaana na Namungo FC kwenye mechi ya Ngao ya Jamii ambayo ni maalum kwa ajili ya kukaribisha msimu mpya wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Septemba 6, mwaka huu.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
20h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’