Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba kitaondoka jijini Dar es salaam leo Ijumaa kuelekea mkoani Arusha tayari kwa mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopiwa Jumapili, August 30
Mchezo huo dhidi ya Namungo Fc, utakuwa wa kufungua msimu mpya wa ligi 2020/21 na utapigwa kuanzia saa tisa na nusu Alasiri
Mabingwa hao wa nchi wamekamilisha maandalizi yao ya mwisho leo asubuhi katika uwanja wao wa Mo Simba Arena tayari kwa safari
Miongoni mwa wachezaji ambao watajumuishwa kwenye msafara wa kikosi cha Simba ni beki kisiki Paschal Wawa na kiungo mshambuliaji Luis Miquissone ambao walitua jana wakitoka kwenye 'fungate' baada ya kufunga ndoa
ADVERTISE HERE