Nyota wawili wa klabu ya Simba Luis Miquissone na Paschal Wawa wamerejea nchini na moja kwa moja kuungana na kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumapili mkoani Arusha
Taarifa iliyotolewa na Simba imebainisha kuwa wachezaji hao watajumuishwa kwenye safari ya mkoani Arusha
"Luis Miquissone na Pascal Wawa wamerejea nchini na watakuwa sehemu ya kikosi ambacho kitaenda jijini Arusha kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo FC ambao utapigwa jumapili Agosti 30, 2020," taarifa ya klabu ya Simba imebainisha
Miquissone na Wawa walipewa ruhusa ya kurejea katika nchi zao kwenda kufunga ndoa
ADVERTISE HERE