Chama alenga mafanikio zaidi msimu huu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Aug 2020
Chama alenga mafanikio zaidi msimu huu

Kiungo wa Simba Clatous Chama amesema msimu huu wachezaji wanapaswa kupambana ili kuhakikisha wanafikia mafanikio waliyopata msimu uliopita au zaidi

Msimu uliopita ulikuwa wa mafanikio zaidi kwa mabingwa hao wa nchi wakitwaa mataji yote kuanzia Ngao ya Jamii, Ligi kuu na kombe la FA

Chama aliibuka kuwa mchezaji na kiungo bora wa msimu

Wakati huu ambao Simba inajiandaa kuanza kampeni ya msimu mpya kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo Fc siku ya Jumapili, Chama amesema hawapaswi kubweteka

"Hatupaswi kulewa kwa mafanikio ya msimu uliopita, tunapaswa kujituma ili kuweza kufanikiwa tena," alisema Chama

"Tuna timu nzuri hivyo natarajia tutakuwa na msimu mwingine wa furaha kwa mashabiki wetu"

Simba imecheza mechi tatu za kujipima na kufanikiwa kushinda zote

Waliwafumua Vital'o 6-0, KMC 3-1 na Transit Camp 5-2

Baada ya mchezo dhidi ya Namungo Fc, wataenda kuanzia ligi mkoani Mbeya kwa wakiifuata Ihefu Fc Septemba 06

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’