Winga wa Simba Rashid Juma amepelekwa kwa mkopo klabu ya Polisi Tanzania ya kule mkoani Kilimanjaro
Juma ataitumikia timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja, Polisi Tanzania wamethibitisha
"Kwa furaha kubwa tunapenda kumtambulisha Winga Rashid Juma kutoka Simba Sc"
"Rashid amekuja kwa mkopo wa mwaka mmoja. Ni mchezaji mwenye kipaji na tunaamini akiwa hapa Polisi Tanzania atafanya vizuri zaidi. Karibu sana Rashid Juma ndani ya uwanja wa Ushirika Moshi"
Juma anakuwa mchezaji wa pili kutolewa kwa mkopo na Simba akitanguliwa na Shiza Kichuya aliyepelekwa Namungo FC
Hii ni nafasi muhimu kwake kuimarisha kiwango chake na kulinda kipaji alichonacho
ADVERTISE HERE