Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kiungo Gerson Fraga aliomba ruhusa arejee kwao Brazil kushughulikia matatizo ya kifamilia, atarejea nchini baada ya siku chache
Kumekuwa na sintofahamu kuhusu Fraga ambaye alirejea nchini wiki iliyopita huku kukiwa na taarifa kuwa awali aliomba aachwe kwenye kikosi cha msimu huu
"Fraga bado yuko nasi, aliniomba ruhusu arudi kwao (Brazil) kwenda kushughulikia matatizo ya kifamilia, atarejea siku chache zijazo," alisema Sven jana
Hatma yake itafahamika ndani ya siku tatu kwani kama ameondoka moja kwa moja Simba italazimika kusajili mbadala wake kabla ya August 30 siku ambayo dirisha la usajili litafungwa
Β
ADVERTISE HERE