Mwishoni mwa wiki hii siku ya Jumapili, mabingwa wa nchi hii Simba watakuwa kule mkoani Arusha kusaka taji la kwanza msimu huu watakapoumana na Namungo Fc katika mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) mapema leo waliweka wazi muda wa mchezo huo kuwa utapigwa saa tisa Alasiri
Simba mabingwa wa Ngao ya Jamii kwa misimi mitatu mfululizo watakuwa wakisaka Ngao ya nne
Lakini pia huo utakuwa mchezo wa kwanza kabisa msimu huu, ukiwa maalum kwa ajili ya kuzindua msimu mpya
Baadae Simba itaelekea mkoani Mbeya kuifuata Ihefu kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa ligi utakaopigwa Septemba 06
ADVERTISE HERE