Fraga humwambii kitu kwa Bwalya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Aug 2020
Fraga humwambii kitu kwa Bwalya

Kiungo wa Simba, Gerson Fraga Vieira raia wa Brazil amesema kuwa usajili wa kiungo mpya, Larry Bwalya kutokea Klabu ya Lusaka Dynamos ya nchini Zambia ni miongoni mwa usajili bora ambao umefanyika

Fraga ameeleza kuvutiwa na uwezo mkubwa anaouonyesha kiungo huyo katika viwanja vya mazoezi vya Simba Mo Arena vilivyoko Bunju jijini Dar.

Simba ilianza rasmi mazoezi ya kujiandaa na msimu wa 2020/21, Agosti 17 huku wachezaji wote saba wapya wakiwa sehemu ya mazoezi hayo na kuwapagawisha mashabiki wa timu hiyo ambao wamekuwa wakikusanyika kwa wingi kuwashuhudia.

"Naupongeza uongozi kwa usajili bora ambao wameufanya kuelekea msimu ujao, baada ya kupata nafasi ya siku chache kufanya mazoezi na nyota wapya waliosajiliwa kwa upande wangu nadhani usajili huu utazidi kutufanya bora zaidi.

"Nimevutiwa sana na uwezo mkubwa wa kiungo wetu mpya, Larry Bwalya ambaye amekuwa kivutio kikubwa kutokana na kipaji cha soka alichonacho, naamini tutakuwa imara zaidi tutakapocheza pamoja," amesema Fraga.

Bwalya amekuwa kipenzi cha mashabiki kwa muda mfupi kutokana na uwezo wake anaounyesha ndani ya uwanja. Kwenye tamasha la Simba day, Agosti 22 alikuwa ni miongoni mwa nyota waliofanya vizuri mchezo wa kwanza wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Vital'0 ya Burundi.

Simba ilishinda mabao 6-0 yeye alitoa pasi moja ya bao lililopachikwa kimiani na Bernard Morrison. Fraga pia alikuwa miongoni mwa viungo waliofanya vizuri

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’