Kiungo wa Coastal Union Athumani Iddi 'Chuji' ameifungia timu yake bao muhimu kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mawenzi na kufanikiwa kurejea ligi kuu ya Vodacom.
Chuji aliyejizolea umaarufu wakati akivitumikia vilabu vya Simba na Yanga, amekuwa chachu ya mafanikio kwa Coastal iliyorejea ligi kuu baada ya kusota kwa misimu miwili.
Nayo KMC inayonolewa na mkongwe Fred Felix Minziro imepanda daraja baada ya kuilaza JKT Mlale bao 1-0.
KMC imemaliza kundi B ikiwa na nafasi ya kwanza baada ya kufikisha alama 28 ikifuatiwa na Coastal Union yenye alama 26.
Timu hizo zinaungana na JKT Ruvu kuwa timu tatu za kwanza kupanda ligi kuu ya Vodacom msimu ujao.
Timu sita zinatarajiwa kupanda daraja huku mbili zikishuka kutoka ligi kuu msimu huu.
Msimu ujao timu 20 zitashiriki ligi kuu ya Vodacom.

ADVERTISE HERE