Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita Clatous Chama 'CCC' Mwamba wa Lusaka, amesema usajili wa kiungo wa Kimataifa wa Zambia Larry Bwalya katika klabu ya Simba, sio tu utakuwa na faida kwenye ligi, lakini hata kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Bwalya ametua Simba akitokea klabu ya Power Dynamos ya Zambia, juzi alionyesha ubora wake kwenye mchezo wa utambulisho wa kikosi dhidi ya Vital'o na Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 6-0
Chama amesema anamfahamu vizuri Larry, mashabiki wasubiri burudani kutoka kwake
"Bwalya ataisaidia timu kwa kiasi kikubwa, sio tu katika Ligi ya Tanzania lakini pia wakati tunapoanza safari yetu kwenye Ligi ya Mabingwa CAF"
"Ni ongezeko bora kwa timu, ana uzoefu wa kucheza katika hatua zote mbili, ligi na mashindano ya CAF, na ninafurahi tutaweza kupata mchango wake.
Chama na Larry wamekuwa wakicheza pamoja
"Ninamjua vizuri na naamini kabisa anakuja kuwa msaada mkubwa ndani ya timu," alisema Chama