Wapo wlaiokuwa wakibeza usajili wa beki kisiki Joash Onyango kuwa umri umemtupa mkono licha ya ukweli kuwa na umri wa miaka 27 tu
Lakini kile alichofanya kwenye mchezo dhidi ya Vital'o jana ni salamu tosha kwa wale wakosoaji wa upande wa pili
Huyu ni beki kwelikweli. Mtu unapata wapi ujasiri wa kumbeza mchezaji aliyeitumikia Gor Mahia klabu bingwa ya Kenya kwa mafanikio makubwa na pia akiitumikia timu ya Taifa?
Beki huyu kisiki ameletwa Simba kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa ambako Simba imeweka mkazo zaidi
Ni beki anayeonekana kumudu mikiki mikiki ya mechi ngumu, mechi ya jana ilikuwa rahisi sana kwake
Lakini pia alianza vyema na Mzanzibar Ibrahim Ame. Bila shaka ndani ya Simba, Ame anakwenda kuwa mmoja wa mabeki bora nchini
Pengine wakati alipokuwa Coastal Union hakupewa sifa anazostahili, vyombo vya habari vikimbeba zaidi pacha wake Bakari Nondo Mwamnyeto