Licha ya ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Vital'o ya Burundi kwenye mchezo wa Simba Day hapo jana, kocha mkuu wa mabingwa wa nchi Sven Vandenbroeck amesema kikosi chake bado hakijaiva sawasawa kutokana na muda mdogo wa maandalizi
Sven amesema watatumia wiki nyingine moja kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza kabla ya mchezo dhidi ya Namungo Fc Jumapili ijayo
"Tumefurahi kupata ushindi leo, ilikuwa siku muhimu kuwapa furaha mashabiki wetu. Yapo mapungufu nimeyaona, hakukuwa na muda mrefu wa maandalizi ila ilibidi kupambana"
"Kwa sasa tunatazama yanayofuata ikiwa ni pamoja na mchezo wetu wa ngao ya jamii dhidi ya Namungo, " alisema Sven
Simba itacheza na Namungo August 30 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa mkoani Arusha na baadae kuelekea mkaoni Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya dhidi ya Ihefu Fc