Mo afunguka mikakati mipya Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Aug 2020
Mo afunguka mikakati mipya Simba

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amesema wameweka malengo ya kuhakikisha wanacheza hatua ya makundi ligi ya mabingwa msimu huu lengo kuu likiwa kutwaa ubingwa huo wa Afrika

Mo alizungumza na Wanahabari ofisini kwake mapema leo akielezea mikakati ya mabingwa hao wa nchi

"Mimi siridhishwi na kushinda tu ubingwa wa ndani. Malengo yangu ni ubingwa wa Afrika. Malengo yetu sasa ni kuendelea kushindana ndani na kushinda ubingwa lakini pia kufika kwenye hatua ya makundi ya Ligi ha Mabingwa Afrika"

Aidha Mo amedokeza kuhusu ujenzi wa Hostel kule Bunju uwanja wa Mo Simba Arena pamoja na kuanzishwa kwa Academy

"Mipango yetu mwaka huu ni kujenga hosteli za timu, uwekezaji wa GPS ambao tutakuwa tunaona takwimu za wachezaji"

"Tutaanzisha akademi, kutakuwa na watu ambao watazunguka nchini kutafuta vipaji. Ambao watachaguliwa tutawaleta Dar na tutamgharamia. Tutakuza kipaji chake na tutamlipia gharama za shule."

Mo pia alizungumzia mchakato wa Mabadiliko ambapo amekiri bado haujakamilika lakini ameendelea kuipatia klabu ya Simba takribani Tsh Bilioni tatu kila mwaka kwa ajili ya kujiendesha

"Mfumo wa mabadiliko bado haujakamilika. Bilioni 20 zipo, kwasasa kila mwaka natoka bilioni 3 kama ruzuku kwa klabu. Naamini asilimia kubwa ya Wanasimba wananielewa."

Aidha Mo amesema siku chache zijazo watatangaza nafasi mbalimbali za kazi, moja ya nafasi hiyo ikiwa Mkurugenzi wa Ufundi

Amewataka wanachama na mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kesho Simba Day akiahidi sapraizi nyingine

"Kesho kwenye SIMBADAY2020 kutakuwa na surprise haijawahi kutokea."

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
4m ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
26m ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
3h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
23h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’