Asubuhi ya leo Alhamisi, August 20, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji akiongozana na Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara pamoja na CEO wa Wasafi Nasibu Abdul 'Diamond Platinumz', watakuwa mbashara kwenye kipindi cha michezo cha Sport Arena
Wakati zikiwa zimebaki siku mbili kuelekea kilele cha tukio la Wiki ya Mabingwa, Mwekezaji huyo wa Mabingwa wa nchi anatarajiwa kufunguka mengi kuhusu maandalizi ya tukio hilo la kihistoria
Aidha Diamond Platinumz, yeye aliwaahidi sapraizi mashabiki wa Simba ikielezwa ametunga wimbo maalum kwa ajili ya Simba na Wanamsimbazi wote
ADVERTISE HERE