Manara awatahadharisha wanaozurura mitaani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Aug 2020
Manara awatahadharisha wanaozurura mitaani

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema mabingwa hao wa nchi kwa misimu mitatu mfululizo wamedhamiria kutwaa ubingwa kwa msimu wa nne ndio maana wamekamilisha usajili mapema na tayari wameanza mazoezi

Manara amewataka wapinzani wao Yanga waanze kuandaa malalamiko yao mapema kwani ligi itakapoanza hawatakuwa na huruma

"Waambieni hao wanaozurura huko mitaani waandae kabisa malalamiko, na safari hii wasiwasingizie waamuzi. Mmeona sisi tumesajili tayari na timu yetu imeshaingia kambini, lakini naona wao wanazurura tu. Halafu ligi ikianza wanaanza kulalamika kuwa wanaonewa na hata kuwatwisha mzigo wa lawama waamuzi"

"Tunawaambia sisi tuko makini, ligi itakapoanza kila mmoja ataelewa nini tunamaanisha na hatutaki malalamiko kutoka kwa timu yoyote" alitamba Manara

Kikosi cha Simba kiliingia kambini tangu juzi Jumatatu kujiandaa na mchezo wa Simba Day dhidi ya Vital'o ambao utapigwa Jumamosi ijayo

Lakini pia mabingwa hao wa nchi wanakabiriwa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo Fc August 30 wakati mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa ligi wataanzia ugenini dhidi ya Ihefu Fc Septemba 07 mkoani Mbeya

Β 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’