Viingilio Simba Day hadharani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Aug 2020
Viingilio Simba Day hadharani

Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amesema maandalizi kuelekea kilele cha wiki ya Mabingwa, SIMBA DAY siku ya Jumamosi, August 22 yanaendelea vizuri

Akizungumza na Wanahabari leo katika Mkutano uliofanyika Hoteli ya Serena, Manara amesema uamuzi wa kuileta Vital'o ya Burundi ulifikiwa baada ya kuzikosa baadhi ya timu wakiwemo mabingwa wa kihistoria ligi ya mabingwa Al Ahly, kutokana na changamoto ya corona

Hata hivyo amesema Vital'o sio timu ya kubeza na anaamini watawapa changamoto mabingwa hao wa Tanzania Bara

"Tulipanga kucheza na Al Ahly lakini changamoto ya corona imefanya jambo hilo kuwa gumu. Tunaamini Vital'O itatupa changamoto nzuri kwenye mchezo huo," alisema

"Vital'O itafika ijumaa saa 5 asubuhi na jioni timu zote zitafanya mazoezi kwenye uwanja wa Mkapa"

Manara amesema siku hiyo burudani zitakuwa nyingi kutoka kwa wasanii mbalimbali walioalikwa lakini kubwa zaidi atakuwepo Diamon Platinumz, moja wa mabalozi wa Simba, yeye akiwa na zawadi maalum kwa mashabiki wa Simba

"Burudani itatolewa na Twanga Pepeta, Tunda Man, Meja Kunta, Mwasiti na kipekee atakuwepo Diamond Platinumz. Litakuwa kama tamasha la mziki, amekusudia kufanya jambo kubwa na kwa kupitia hilo kesho alhamisi kutakuwa na BIG SURPRISE kwa Wanasimba. MC atakuwa Mpoki."

Aidha akitaja viingilio vya tukio hilo, Manara watatumia viwanja viwili, Uwanja wa Mkapa na Uwanja wa Uhuru

Kwa mashabiki watakaoingia uwanja wa Uhuru watalipa Tsh 2,000/- na watapata fursa ya kuona kila linaloendelea ndani ya uwanja wa Mkapa

Aidha wachezaji wataanzia uwanja wa Uhuru kuwasalimia mashabiki kabla ya kuelekea uwanja wa Mkapa

Viingilio vya Uwanja wa Mkapa;

Mzunguko: 7,000/=
VIP C: 20,000/=
VIP B: 30,000/=
VIP A: 40,000/=
Platinum tickets: 150,000/=

Kwa mashabiki 10 wa mwanzo ambao watanunua tiketi za Platinum, watapata fursa ya kushiriki hafla maalum ambayo itafanyika usiku ikiwahusisha wachezaji pamoja na viongozi wa Simba na Vital'o

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’