Larry afurahia kucheza na Chama

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Aug 2020
Larry afurahia kucheza na Chama

Kiungo mpya wa Simba Larry Bwalya amesema uamuzi wa kujiunga na Simba ulikuwa rahisi kwake baada ya kupokea ofa kutoka kwa mabingwa hao wa nchi

Awali Bwalya alikuwa akitajwa kuwa mbioni kusajiliwa na Yanga lakini siku ambayo alipaswa kutua Yanga, kupitia wakala wake, Simba waliweza kupindua meza na kumvuta Msimbazi kuungana na Mzambia mwenzake Clatous Chama

"Nilipotaarifiwa na Wakala wangu kuwa Simba wananihitaji sikufikiria mara mbili. Ni klabu yenye historia kubwa hivyo nilipenda kuwa sehemu ya historia hiyo," alisema Larry

Aidha nyota huyo ameeleza kufurahi kucheza na Chama katika klabu moja, licha ya kuwa walikuwa wakikutana katika timu ya Taifa ya Zambia

"Nafurahi kucheza na Chama katika timu moja kama tunavyofanya timu ya Taifa. Naamini kwa ushirikiano na wachezaji wenzetu pamoja na sapoti ya mashabiki tutafanya vizuri"

Simba imemsajili Bwalya kuchukua nafasi ya Sharaff Shiboub ambaye mkataba wake umemalizika

Ni kiungo fundi box-2-box ambaye anazimudu vyema nafasi zote za kiungo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’