Mabingwa wa nchi Simba walianza rasmi mazoezi jana kuelekea kilele cha wiki ya Mabingwa, Simba Day siku ya Jumamosi
Katika mazoezi hayo ya kwanza, nyota wote saba waliosajliwa katika dirisha hili la usajili walishiriki
Winga Bernard Morrison aliyetokea klabu ya Yanga alikuwa kivutio kwa mamia ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mazoezi hayo
Mwamba huyo kutoka Ghana hakuacha kuonyesha utaalam wake wa kutembea juu ya mpira, na hakusita kupiga picha na mashabiki waliokuwa wakishangilia kila alichokuwa akifanya
Morrison amejiunga na timu iliyojaa mafundi kwelikweli. Bila shaka atakuwa na nafasi ya kuonyesha makali yake zaidi ya kule alikotoka ambako ni yeye tu aliyekuwa mchezaji tegemeo
ADVERTISE HERE