Mabingwa wa soka Tanzania Bara kwa misimu mitatu iliyopita, Simba wataianza kampeni ya kusaka ubingwa wa nne mfululizo kwa kuikabili Ihefu Fc katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu msimu wa 2020/21
Kulingana na ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi mapema leo, Septemba 06 Simba watasafiri mkoani Mbeya kuwafuata Ihefu Fc katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Sokoine
Kabla ya mchezo huo, Simba itaanza msimu mpya kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa August 29 mkoani Arusha
Aidha, Mchezo wa kwanza ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga, umepangwa kupigwa Oktoba 18 mwaka huu, Uwanja wa Taifa wa Mkapa, Jijini Dar es Salaam
Ratiba ya mechi za raundi ya kwanza;

ADVERTISE HERE