Okwi awaambia Ruvu Shooting wajiandae kisaikolojia

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Feb 2018
Okwi awaambia Ruvu Shooting wajiandae kisaikolojia
Mshambuliaji kinara wa mabao kwenye kikosi cha Simba Emanuel Okwi amesema wamejiandaa kuendelea na kasi ya upachikaji mabao watakapoivaa Ruvu Shooting kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 16 Jumapili, Februari 04.

Timu hizo zilipokutana kwenye duru ya kwanza, Ruvu Shooting ilitota kwa mabao 7-0 huku Okwi kifunga mabao manne peke yake.

Mshambuliaji huyo wa Kimataifa kutoka nchini Uganda ameahidi kuendeleza kasi yake ya kupachika mabao.

Okwi amefunga mabao 12 kwenye ligi na mabao yote ameyapachika kwenye viwanja vya Taifa na Uhuru. Hivyo upo uwezekano mkubwa wa yeye kuendelea kufunga katika mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa taifa.

Hata hivyo Ruvu Shooting nayo imekamia kulipa kisasi. Msemaji wa klabu hiyo mwenye maneno mengi Masau Bwire amesema Simba isifikiri inakutana na Ruvu Shooting ya mzunguuko wa kwanza.

Katika mzunguuko wa kwanza, Bwire amesema wachezaji karibu wote wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo walikuwa nchini Burundi kushiriki michuano ya majeshi.

Lakini katika mchezo ujao watakuwa na kikosi chao kamili kuweza kutoa upinzani kwa vinara wa ligi, Simba.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
15h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
18h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’