Klabu ya Simba imetambulisha usajili wa beki kisiki Ibrahim Ame kutoka klabu ya Coastal Union
"Ni beki aliyekamilika, bahati mbaya sio macho ya watu wote waliokuwa wamemwelewa ila benchi la ufundi la Simba likatwambia pale Coastal Union tunamtaka Ame"
"Unajua nini hoja yao? Ni beki mpambanaji mno, mzuri juu na chini na anayo ile akili ya Kizanzibar ya ujeuri uwanjani."
βͺ"Beki mahiri lazima uwe na ujasiri. Karibu Ame kwa mabingwa wa taifa lako. Umechagua sehemu sahihi na yenye uhakika wa malipo na vikombe," ilisema taarifa ya Simba

ADVERTISE HERE