Jumamosi ijayo, August 22 Simba itakamilisha wiki ya Mabingwa kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya moja ya vilabu kutoka nje ya nchi
Mwaka jana Simba walicheza na Power Dynamos ya Zambia na mwaka huu inaelezwa Simba watacheza na klabu nyingine kutoka nchini Zambia, Zanaco Fc
Katika Tamasha la Mwaka huu, Simba imeomba viwanja viwili, Uwanja wa Mkapa na Uwanja wa Uhuru ili kuwapa fursa mashabiki wengi kushiriki katika tukio hilo
Uwanja wa Uhuru kutaweka TV kubwa ambayo itaonyesha matukio yote yatakayokuwa yakiendelea uwanja wa Mkapa
Hivyo kwa mashabiki ambao watashindwa kuingia uwanja wa Mkapa, watapata fursa ya kufuatilia kila kinachoendelea pale uwanja wa Uhuru
ADVERTISE HERE