Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, amethibitisha kuwa mchezo kati ya Simba na Azam FC unaotarajiwa kufanyika Februari 7, mwaka huu, utafanyika kama ulivyopangwa na ule wa ugenini dhidi ya Mwadui FC ndio umesogezwa mbele.
Hivyo Baada ya mchezo dhidi yaAzam FC, vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara watajiandaa kuwakaribisha Gendarmarie Nationale katika mchezo wa kwanza wa raundi ya awali ya mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho.
Mchezo huo utapigwa Jumapili, Februari 11 kwenye dimba la Taifa.
Kwa sasa Simba inajiandaa na mchezo wa ligi mzunguuko wa 16 dhidi ya Ruvu Shooting.
Simba inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia pointi 35 na ni timu pekee ambayo haijafungwa katika mechi za mzunguko wa kwanza wakifuatiwa na Azam FC wenye pointi 30, mabingwa watetezi, Yanga wao wana pointi 28 na Singida United yenye pointi 27 wako katika nafasi ya nne kwenye msimamo.

ADVERTISE HERE