Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza usajili wa aliyekuwa beki kisiki wa Gor Mahia na timu ya Taifa ya Kenya Joash Onyango
Onyango ametua Simba akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na Gor Mahia
Ni mchezaji wa pili kutambulishwa leo baada ya mshambuliaji Charles Ilanfya
"Tumeweka malengo makubwa msimu huu ya kufika mbali kwenye ligi ya Mabingwa Afrika na mashindano ya nyumbani hivyo lazima pia klabu isajili mabeki na wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika mechi kubwa kubwa. Beki wa kimataifa wa Kenya, Joash Onyango ametua Msimbazi," imesema taarifa ya Simba

ADVERTISE HERE