Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania kupitia kwa Mwenyekiti wake, imwasilisha Malalamiko katika Kamati ya Maadili dhidi ya Wanafamilia watatu wa mpira wa Miguu kwa kuchochea hisia za Jamii na kutoa vitisho kuhusu shauri lililokuwa mbele yake
Wanafamilia hao ni Mjumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF Zacharia Hans Poppe, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara na mchezaji Bernard Morrison
Pia Sekretarieti ya TFF imempeleka Mkuu wa idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Hassan Bumbuli katika Kamati ya Maadili kwa kutoa taarifa ya uongo
Wahusika watapewa Malalamiko dhidi yao kwa njia ya Maandisi pamoja na wito wa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Maadili

ADVERTISE HERE