Kwanza leo ni uzinduzi wa wiki ya Mabingwa (Simba Chmpions Week) ambapo mabingwa wa nchi, Simba wanazindua rasmi lile tukio ambalo wameliasisi na kulifanya kila mwaka tangu mwaka 2009
Katika wiki hii Wanasimba watashiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii, kilele chake kikitarajiwa kuwa August 22 kwa mchezo wa kirafiki ambao Simba itacheza na moja ya vilabu kutoka nje ya nchi
Mchezo huo utapigwa uwanja wa Taifa, lakini Simba imeomba kuweka TV kubwa kwenye uwanja wa Uhuru ili kuwapa fursa mashabiki ambao watakosa nafasi ya kuingia uwanja wa Taifa kwani ni kawaida uwanja huo hufurika na mashabiki wengi kukosa fursa ya kushuhudia burudani
Lakini pia leo Simba itatangaza wachezaji wapya ambao wamesajiliwa mpaka sasa
Usajili huu Simba imebadili utaratibu wa kutambulisha wachezaji. Pamoja na kuhusisha kumalizana na baadhi ya nyota, bado klabu haijatoa taarifa rasmi
Zoezi hilo litafanyika kuanzia leo
Jambo kubwa la tatu ni utambulisho wa jezi mpya kwa ajili ya msimu wa 2020/21 unaoanza Septemba 06
Wansimba wako tayari kununua jezi, bila shaka baada ya utambulisho huo jezi zitaanza kupatikana leoleo