Haya huku Morrison, kule Miquissone sijui itakuwaje?

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Aug 2020
Haya huku Morrison, kule Miquissone sijui itakuwaje?

Kwa sasa mashabiki wa Simba wana haki ya kushangilia baada ya kuwa na uhakika na huduma ya winga msumbufu Bernard Morrison ambaye leo Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imemtangaza kuwa mchezaji huru baada ya kushinda kesi yake ya mkataba dhidi ya Yanga

Morrison alisaini mkataba wa kujiunga na Simba August 08 hata hivyo kulikuwa na hofu ya maamuzi ya kesi yake dhidi ya Yanga ambayo imechukua siku mbili

Sasa ni rasmi Morrison atakuwa ndani ya uzi wa klabu ya Simba kuanzia August 29 pale Simba itakapocheza na Namungo Fc kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii

Hili ni tatizo lingine kwa timu pinzani msimu ujao kwani, kama Mmakonde Luis Miquissone aliwachachafya vile itakuwaje akikutana na Morrison kwenye timu moja?

Kwa wale wanaodhani Morrison atafanya vituko kama alivyokuwa akiwafanyia Yanga wasahau, kwani mwenyewe anafahamu amejiunga na taasisi imara ambayo inafuata na kuheshimu misingi yake

Ndani ya Simba Morrison atapatiwa mahitaji yake yote, hivyo hatakuwa na sababu ya kufanya migomo na matukio mengine ya utovu wa nidhamu

Tukutane ligi ya mabingwa...!

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
17h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
18h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
21h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’