Magori awashangaa wanaovumisha tetesi kumuhusu Chama

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Aug 2020
Magori awashangaa wanaovumisha tetesi kumuhusu Chama

Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba, Crescentius Magori ameeleza kushangazwa na tetesi nyingi zinazomuhusu kiungo wao Mzambia Clatous Chama kuwa amesajiliwa na Yanga

Magori amesema Chama aliyeibuka kuwa kiungo na mchezaji bora wa VPL msimu wa 2019/20, ni mchezaji halali wa Simba na bado ana mkataba na mabingwa hao wa nchi

CEO huyo wa zamani wa Simba amesema katika hali ya kawaida wangekuwa viongozi wajinga kama wasingemuongezea mkataba kutokana na ubora alionao

"Hivi katika hali ya kawaida unafikiri Simba inaweza ikamuacha tu Chama acheze bila ya kuwa na mkataba mrefu? Hatuwezi kufanya hivyo, Wanasimba hata wasiwe na wasiwasi Chama ni mchezaji wetu halali. Kama kuna timu inamtaka basi waje mezani na sio chini ya dola 800,000 tunaweza kufikiria kuwauzia," alisema Magori

Baada ya Simba kutangaza usajili wa winga Bernard Morrison, taarifa zikasambazwa kwenye mitandao ya kijamii mashabiki wa Yanga wakitamba kuwa wamemsajili kiungo huyo fundi

Msimu uliopita Chama aliongeza mkataba wa miaka miwili ambao utamalizika Julai 21 2021

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’