Beki kisiki wa timu ya Gor Mahia na timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars, Joash Onyango, amekubali kutua klabu ya Simba
Onyango anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa nchi
Taarifa ambazo zimethibitishwa na vyombo vya habari nchini Kenya, zimebainisha kuwa Onyango ameridhia kusaini mkataba wa miaka miwili
Ujio wa Onyango huenda ukaweka shakani hatma ya walinzi wakongwe Paschal Wawa na Erasto Nyoni Simba pia ikiwa tayari imemsajili beki Ibrahim Ame kutoka klabu ya Coastal Union
ADVERTISE HERE