Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba,Hajji Manara ametoa angalizo kwa Mwenyekiti wa kamati ya TFF inashughulikia mgogoro wa mkataba wa mchezaji Bernard Morrison na Yanga, kutenda haki la sivyo wataingia matatizoni.
Manara amemtaka mwenyekiti wa kamati hiyo Elius Mwanjala kutoa maamuzi yaliyonyooka na kusikiliza hoja iliyo mezani inayohusisha kufojiwa kwa mkataba wa nyota huyo raia wa Ghana.
Aidha, Manara amesema Serikali ya Rais wa nchi Dk John Magufuli ipo macho na inafuatilia Mambo Kama haya,huku akitoa angalizo kuwa watu wakileta mzaha watafungwa kama ilivyokua kwa aliyekuwa Rais wa TFF, Jamali Malinzi.
Manara ameongeza kuwa utawala huu sio kama wa awamu zilizopita, Takukuru, na taasisi zote zinachungulia suala hili, hivyo watu wasilete mzaha
Hukumu ya hatma ya Morrison inatarajiwa kutangazwa leo, saa nane mchana