Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba kinatarajia kuingia kambini Jumatatu ijayo kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi, igi ya mabingwa na michuano ya kombe la FA, imefahamika
Ligi Kuu itaanza Septemba 06 lakini kabla ya hapo mwishoni mwa mwezi huu August 29, Simba itashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha kuumana na Namungo Fc katika mchezo wa Ngao ya Jamii
Baada ya kumaliza msimu kibabe kwa kutwaa mataji yote, wachezaji wa mabingwa hao wa nchi walipewa mapumziko ya wiki mbili
Viongozi wa Simba kwa sasa wanaendelea na michakato ya usajili pamoja na mingine ya ndani wakisubiriwa kumtangaza mrithi wa Senzo Mazingisa aliyetimkia Yanga juzi
ADVERTISE HERE