Okwi kuhamishia makali kombe la Shirikisho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
31 Jan 2018
Okwi kuhamishia makali kombe la Shirikisho
Baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting wiki ijayo, kikosi cha Simba kitakuwa na wiki moja kujiandaa na mchezo wa hatua ya awali michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Gendarmeri ya Djibouti.

Mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Taifa Februari 11, siku moja baada ya watani zao Yanga kuumana na St Louis kwenye michuano ya ligi ya mabingwa.

Kinara wa mabao kikosi cha Simba Emanuel Okwi amesema wanapaswa kufanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Wasibweteke na mafanikio wanayopata kwenye ligi kuu ya Vodacom.

Okwi amesema matokeo mazuri inayopata Simba katika Ligi Kuu sio kigezo cha timu hiyo kufanya vyema katika Kombe la Shirikisho.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uganda, anaongoza kwa kufunga mabao 12 katika Ligi Kuu yaliyochangia Simba kubaki kileleni kwa pointi 35.

“Tunafurahi tumekuwa na mwenendo mzuri kwenye ligi, sifa zinakwenda kwa timu nzima si mimi kufunga mabao na jambo la msingi ni kuongeza juhudi katika maandalizi ya mashindano ya kimataifa,”alisema mshambuliaji huyo mwenye kiwango bora msimu huu.

Okwi amesema kila mchezaji anatakiwa kuweka malengo ya kucheza kwa kiwango bora mashindano ya kimataifa mwaka huu.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →