Mjumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji Zacharia Hans Poppe ameeleza kushangazwa na muda mrefu uliochukuliwa na kamati hiyo kutangaza mwafaka wa sakata la winga Bernard Morrion aliyejiunga na Simba akitokea klabu ya Yanga hivi karibuni
Aidha Poppe amemtuhumu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Elias Mwanjala kuwa ameweka 'unazi' wake wa Yanga mbele na ndio maana suala hilo limechukua muda mrefu kutangazwa
"Nashangaa kwa nini maamuzi yachukue muda mrefu kiasi hiki, kesi hii haikupaswa kuchukua hata saa moja kwani ushahidi na kila kitu kiko wazi. Huyu Mwenyekiti anajaribu kupindisha mambo jambo ambalo haliwezekani. Mbili jumlisha mbili ni nne hata siku moja haiwezi kugeuka kuwa tano," alisema Poppe katika mahojiano na Wasafi Fm mapema leo
Poppe ni miongoni mwa wajumbe wa Kamati hiyo ambayo ilikutana jana tangu saa tano asubuhi mpaka kufikia usiku wakawa hawajapata mwafaka na kuahirisha kutangazwa kwa maamuzi mpaka siku ya leo saa nane mchana
Morrison amedai alianza kuitumikia Yanga pasipo kuwa na mkataba halali na hata mkataba mpya anaodaiwa kusaini Yanga amesema hautambui