Inaelezwa uongozi wa klabu ya Simba huenda ukamshusha nchini mlinzi wa kati wa Gor Mahia na timu ya Taifa ya Kenya, Joash Onyago
Awali klabu ya Simba ilikuwa ikimuwania beki wa kimataifa wa Burundi na Klabu ya Chippa United ya Afrika kusini Frederic Nsubaiyumva mwenye umri wa miaka 25.
Klabu ya Simba ilishatuma ofa kwa klabu yake ya Chippa lakini timu hiyo haionekani kuwa tayari kumuachia mlinzi huyo


Onyango anatajwa kumaliza mkataba kunako klabu ya Gor Mahia hivyo anaweza kupatikana kwa urahisi zaidi
Mlinzi huyo ana umri wa miaka 27 kama Simba itafanikiwa kumsajili, atakuwa mchezaji wa tatu kujiunga Simba akitokea klabu ya Gor Mahia katika kipindi cha misimu mitatu
Simba ilianza na Meddie Kagere, msimu uliopita ikamsajili Francis Kahata
ADVERTISE HERE